• This is default featured slide 1 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 2 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 3 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 4 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 5 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Monday, February 27, 2017

HIFADHI YA MAZINGIRA ASILIA YA CHOME




Moja kati ya Vivutio vya Kitalii vilivyopo katika Hifadhi ya Mazingira Asilia Chome/Shengena ni ndege adimu aina ya  “South Pare white eye”.
Hifadhi ya Mazingira Asilia Chome/Shengena inasimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii. Hifadhi hii ilitangazwa katika tangazo la Serikali (GN) Na. 125 la tarehe 25/05/1951 kama msitu wa Hifadhi. Baadaye hifadhi hii ilipandishwa hadhi na kuwa Hifadhi ya Mazingira Asilia kwa tangazo la Serikali Na. 105 la tarehe 25/03/2016. Hifadhi ina ukubwa wa hekta 14,283 na urefu wa mpaka upatao Kilometa 67. Hifadhi inazungukwa na vijiji 27, kata 11 ambapo wakazi wake kwa kiasi kikubwa maisha yao hutegemea uwepo wa hifadhi ya Chome kwa shughuli za kiuchumi na kijamii. Hifadhi hii ina umuhimu mkubwa Kitaifa na Kimataifa kutokana na vyanzo vingi vya maji vilivyopo na utajiri mkubwa wa bioanuwai. Katika kuhakikisha kuna usimamizi mzuri, hifadhi ya mazingira asilia ya Chome imegawanyika katika maeneo (Safu) matano  ya usimamizi ambayo ni Chome, Suji, Mamba myamba, Bombo na Bwambo.


 Hifadhi hii imeanzishwa ikiwa na malengo yafuatayo:

1 .Kutunza mazingira asili, mifumoikologia katika uasilia wake.
2. Kuimarisha uhifadhi wa baioanuwai na mifumoikolojia.
3. Kuimarisha mafunzo na tafiti mbalimbali.
4. Kushirikisha jamii na wadau wote katika kulinda, kuhifadhi na kuendeleza
    uhifadhi.
5. Kuelimsha jamii inayozunguka hifadhi njia mbadala ya kujiongezea kipato katika kupunguza umaskini na kupunguza utegemezi wa hifadhi.

Hifadhi ya mazingira asilia ya chome ni hifadhi yenye umuhimu wa kipekee siyo tu kwa wakazi wa wilaya ya Same bali pia  hata kwa Taifa kwa ujumla. Hifadhi hii ina umuhimu ufuatao:-
 
·         Eneo hili lina bio-anuwai nyingi za mimea na wanyama(ndwele/adimu).   wanaopatikana katika hifadhi hii pekee . mojawapo ya ndege ndwele anaitwa “South Pare white eye”. 

Hifadhi hii, ni kivutio cha utalii wa wanyama, ndege, maporomoko ya maji, maumbile asilia, mimea adimu nk.
·        Eneo hili linatunza maumbile ya asili,  kuboresha hali ya hewa na kuhifadhi gesi ukaa na kuvuta mawingu yanayoleta mvua za mara kwa mara. 

Hifadhi hii ni chanzo cha maji kwa matumizi ya kilimo na chakula kwa jamii na wakazi wanaozunguka hifadhi hii. 

SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA HIFADHI YA MAZINGIRA ASILIA YA CHOME

Ili kuhakikisha kuwa uhifadhi unaendelea na hatimaye kufikia malengo na umuhimu  tajwa hapo juu hifadhi hii inafanya shuguli zifuatazo;

  • Kufanya Doria shirikishi ndani na nje ya Hifadhi kwa kushirikiana na Kamati za Maliasili za vijiji.
  • Kuimarisha mpaka wa hifadhi kwa kusafisha mipaka na kupanda miti kwa lengo la kuepuka wavamizi wa hifadhi na kudhibiti matukio ya moto.
  • Kurejesha maeneo yaliyoharibiwa na wachimbaji madini haramu kwa kufukia mashimo yaliyoachwa wazi, kurudisha mikondo ya maji kwenye njia za asili na kupanda miti.
  •  Kuimarisha miundo mbinu ya  kitalii kwa ajili ya utalii ikolojia.
  • Kuiwezesha jamii inayozunguka hifadhi kuanzisha bustani zao za miti  kwa ajili ya kupanda katika maeneo yao.
  • Kuiwezesha jamii inayozunguka  hifadhi kuanzisha miradi midogomidogo ya kujiongezea kipato mfano ufugaji nyuki,ufugaji wa vipepeo, ufugaji wa samaki , ufugaji wa kuku n.k.
  • Kushirikisha jamii katika shughuli za uhifadhi na utunzaji wa mazingira kwa ujumla
  • Kuandaa mipango ya utekelezaji kazi, usimamizi wa hifadhi na sheria ndogondogo za vijiji
  •  Kutengeneza mabango yanayoelezea eneo la hifadhi na kuyasimika  katika mipaka ya hifadhi
  • Kuweka maboya kwenye mpaka wa hifadhi ili kudhibiti wahalifu kutoka nje ya  hifadhi ya asilai ya Chome

FULSA ZA HIFADHI YA CHOME KWA WANANCHI NA JAMII

(a)    UTALII : Katika kuongoza watalii, wananchi wanapata kipato kwa kuongoza watalii, mfano kata ya Chome wananchi wamenufaika kwa kutembelewa na watalii katika nyumba zao na kuona jinsi wanavyoishi kulingana na tamaduni za Kipare. Aidha watalii wameweza kufadhili baadhi ya watoto wa jamii kuwasomesha shule

(b)    UWEKEZAJI: Kuna fursa za kuwekeza kwenye hifadhi kama kujenga hoteli za kitalii, ufugaji nyuki,ufugaji vipepeo, uwekezaji wa kuanzisha umeme mdogo kwenye maporomoko ya maji ndani na nje ya hifadhi, uwekezaji wa ujenzi wa viwanda vidogo vya maji ya kunywa nk. Aidha wakati wa kujenga miundo mbinu ya utalii mfano hoteli, wananchi wamepata ajira.

(c)    AJIRA: Wananchi wamekuwa na wataendelea kuajiriwa kwa kazi za usimamizi wa hifadhi mfano ufyekeaji wa mipaka ya misitu, usimikaji wa maboya (beacons), parizi za barabara ndani ya hifadhin.k


(d)    KILIMO: Wananchi wanaozunguka hifadhi hulima mazao mbali mbali kama vile tangawizi, vitunguu,iliki,nyanya. Mazao haya ya kilimo wananchi huwauzia wananchi wengine, wafanyakazi na hata watalii wanaotembelea hifadhi ya Chome

(e)    UMWAGILIAJI: Hifadhi asilia ya Chome ni chanzo kikubwa cha maji kwa matumizi ya umwagiliaji wa mazao kama mpunga (mradi wa Ndungu), tangawizi, iliki,vitunguu, nyanya. Kilimo cha mazao tajwa hapo juu ni mkombozi wa wananchi katika kujipatia kipato na kuondokana na umaskini.

CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI HIFADHI YA MAZINGIRA ASILIA YA CHOME

Kwa sababu ya wananchi wanaozunguka hifadhi kutegemea hifadhi katika shughuli za kujiongezea kipato, changamoto zifuatazo zimekwamisha juhudi endelevu za kuhifadhi mfano:

  •  Uchimbaji wa madini ndani ya hifadhi
  • Uchomaji moto
  • Upasuaji wa mbao na ukataji miti
  • Uchungaji wa mifugo ndani ya hifadhi(hii ni kwa kiwango kidogo).
  •  Kuwasha moto makusudi kwa lengo la kukomoana kati ya baadhi ya watu na uongozi wa kijiji. Mfano watu waliozuiwa kulima mirungi wanawakomoa walima vitunguu na tangawizi wanaopata maji kutoka kwenye hifadhi ya Chome
  • Faini ndogo inayotolewa kwa waharibifu wa mazingira na misitu mara wafikishwapo mahakamani
  •  Ushiriki mdogo wa wananchi katika shughuli za hifadhi hii ikiwa ni pamoja na kushidwa kuja kutoa ushahidi mahakamani mara wanapotakiwa kufanya hivyo. Aidha baadhi ya wananchi kukataa kuzima moto kwa kisingizio kuwa jukumu hilo ni la watu wa misitu
  • Wakati mwingine watumishi kushambuliwa na wananchi wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao Mfano doria
 
JITIHADA ZILIZOFANYIKA KATIKA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO ZA UHIFADHI
 
Pamoja na changamoto hizo hifadhi ya mazingira asilia kwa kushirikiana na wadau wengine imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kupambana na changamoto zilizoainishwa hapo juu ambazo zimeonyesha mafanikio yafuatayo:

  •  Kwa kufanya doria shirikishi tumefanikiwa kuwaondoa wachimbaji wa madini ndani ya hifadhi. Bado jitihada zinaendelea ili kudhibiti uvamizi huu na kuumaliza kabisa.
  • Upasuaji mbao umepungua  kutokana na doria  shirikishi kati ya watumishi wa misitu na wananchi. Hii imetokana na elimu ya uhifadhi wa misitu tunayowapa jamii inayozunguka hifadhi pamoja na uimarishaji wa sheria ya usimamizi wa misitu ya mwaka 2002 pamoja na sheria ndogondogo za vijiji(Village bylaws)
  •  Kuuongeza ushiriki wa wananchi kwa kuanzisha Kamati za Maliasili za vijiji kwa kila kijiji.ambazo jumla ni 27.
  • Kuimarisha mpaka wa hifadhi kwa kupanda miti na kuweka mabango ili kuzuia uvamizi wa hifadhi.
  • Kuandaa mipango kazi ya usimamizi wa misitu kwa kila kijiji kinachozunguka hifadhi asilia ya Chome
  •  Kuwawezesha wananchi kuanzisha bustani zao za miti ili kupanda katika maeneo yao.
  •  Kuwahamasisha wananchi kutokuwasha moto bila sababu na pindi unapotokea kushiriki kikamilifu kuzima moto.
  • Kutoa mafunzo kwa wananchi juu ya utunzaji wa mazingira

USHIRIKI WA WADAU WENGINE KATIKA UHIFADHI

Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Chome inashirikiana na wadau wafuatao katika kuhakikisha usimaimizi na uhifadhi endelevu wa hifadhi ya Chome/Shengena

·        Ofisi ya Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Same
·        Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same.
·        Ofisi ya Mkuu wa kituo cha polisi Same
·        Mfuko wa hifadhi ya milima ya Tao la mashariki (EAMCEF)
·        Shirika la ONGAWA kupitia shirika la Kuhifadhi Misitu Tanzania (TFCG)
·        Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Mkomazi
·        Serikali na Halmashauri za vijiji
·        Jamii inayozunguka hifadhi ya Mazingira Asilia ya Chome


"Umasikini wa kipato kwa jamii ni changamoto kubwa katika shughuli za uhifadhi wa misitu. Kwa kutumia fursa zilizopo katika jamii inayohusika na kwa kuunganisha nguvu za pamoja na wadau wote uhifadhi endelevu unawezekana kwa ajili ya faida ya wana Same na Taifa kwa ujumla" Mhifadhi Chome.

                                                   


Share:

Tuesday, February 21, 2017

TANZANIA, MSUMBIJI YAKUBALIANA KUTHIBITI UVUNAJI NA USAFIRISHAJI HARAMU WA MAZAO YA MISITU KATIKA MIPAKA YA NCHI HIZO

Kaimu Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu nchini, Dos Santos Silayo (mwenye suti nyeusi) akijadiliana jambo na watendaji wa TFS na Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori na Mazingira Duniani(WWF) Msumbiji, Bi. Anabela Rodriques (mwenye miwani) kabla ya kuanza kwa zoezi la kusaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Msumbiji, jijini Maputo jana kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususan mbao katika mipaka ya nchi hizo mbili. Wengine ni Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi ya Rasilimali wa Wakala wa Misitu nchini Bw. Mohamed Kilongo (mwenye suti) na mwakilishi wa WWF Tanzania, Bw. Geofrey Mwanjelwa.

Kaimu Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu nchini, Dos Santos Silayo (mwenye suti nyeusi) akisaini kusaini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Msumbiji, jijini Maputo jana kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususan mbao katika mipaka ya nchi hizo mbili. Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mazingira na Maendeleo Vijijini, Bi. Sheila Afonso pamoja na mtendaji wa Wizara hiyo (hakuweza kufahamika jina lake mara moja).



Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu nchini imefanya mazungumzo na kusaini hati ya makubaliano na Serikali ya Msumbiji kupitia Wizara ya Ardhi Mazingira na Maendeleo Vijijini mjini Maputo Msumbiji jana kuthibiti uvunaji na usafirishaji wa mazao ya misitu katika maeneo mipaka ya nchi hizi mbili.

Akisaini makubaliano hayo yaliyoratibiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori na Mazingira Duniani(WWF)kupitia mradi wa Crossboaders, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu, Prof. Dos Santos Silayo alisema makubaliano hayo yatasaidia kukabiliana na changamoto za udhibiti wa usafirishaji wa mazao ya misitu hususan mbao katika mipaka ya nchi hizo mbili.

“Makubaliano haya kati ya Tanzania na Msumbiji yatasaidia kupiga vita biashara haramu ya mbao pamoja na mazao ya misitu inayofanyika kupitia mipaka ya nchi hizi, biashara ya uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa za misitu baina ya nchi hizi umekuwa na tija kutokana na kukua kwa soko la nyumba. Hivyo kwa pamoja tukishirikiana tutaweza kuhakikisha sheria, taratibu na kanuni za uzalishaji na usafirishaji wa mazao ya misitu zinafuatwa,” alisema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Mazingira na Maendeleo Vijijini, Sheila Afonso alipongeza hatua hiyo muhimu iliyofikiwa na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kuwa rafiki na ndugu wa dhati wa Msumbiji kama ambavyo mahusiano ya nchi hizi mbili yamejengwa tangu zamani.
Share:

Thursday, February 9, 2017

SHAMBA LA MITI KAWETIRE

Shamba la Miti Kawetire  lipo katika Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani Mbeya, ndani ya msitu wa hifadhi ya Usafwa kaskazini na Safu ya mlima Mbeya. Shamba lipo kilimita 12 kutoka Mbeya mjini katika barabara kuu ya Mbeya – Chunya.

Shamba lilianzishwa mwaka 1937 na serikali ya kikoloni kwa madhumuni ya uzalishaji wa kuni kwa ajili ya migodi ya dhahabu  ya Chunya.

Ili kutimiza azma hiyo miti jamii ya mikaratusi ilipandwa katika eneo la Ipinda. Upanuzi ulifanyika mwaka 1942, 1950 na 1974 kwa kupanda miti jamii  ya misindano (Pinus spp) na mikambokambo (Cupressus lusitanica) na kulifanya shamba lililopandwa kufikia ukubwa kama ilivyo sasa.

Baada ya uhuru madhumuni ya mashamba ya miti likiwemo la Kawetire yaliboreshwa kwenda sambamba na Sera  ya misitu ambayo ni;
  • Kuhakikisha upatikanaji endelevu wa mazao na huduma za misitu kwa kuwa na maeneo ya kutosha na yenye usimamizi madhubuti.
  • Kupanua ajira na kuongeza pato la fedha kutokana na maendeleo endelevu katika viwanda vinavyojikita kwenye misitu.
  • Kuimarisha mifumo ikolojia kwa kuhifadhi bioanuwai ya misitu maeneo ya lindimaji na rutuba ya udongo.
  • Kukuza uwezo wa taifa katika kusimamia na kuendeleza sekta ya misitu kwa kushirikiana na washikadau wengine.
Eneo la Shamba la Miti Kawetire lina msimu mmoja wa mvua ambapo huanza kunyesha mwezi Novemba na kuendelea hadi mwezi  April mwaka unaofuata

Mtiririko unaonesha kwamba miezi ya Juni na Oktoba ni mikavu na kati ya Juni na Agosti ni kipindi cha baridi kali na mara nyingine hali ya joto hufikia nyuzi -5  ̊C hasa wakati wa usiku.

 Kwenye miezi ya joto ya Oktoba na Novemba kiasi cha joto hufikia nyuzi joto 35  ̊C.

Shamba la miti kawetire lina ukubwa wa  hecta 5,280 ambazo zimegawanyika kama ifuatavyo ;

Eneo lililopandwa miti limeongezeka kutoka hekta 1,563 mwaka 2012/2013 hadi hekta 2,720 mwaka 2015/2016 hii inamaanisha upandaji umefanywa katika maeneo mapya kwa ukubwa wa hekta 1,157 kuanzia mwaka 2012/2013 hadi 2015/2016.
Maelezo ya maeneo
Hekta
Eneo lililopandwa miti (mpaka 2012)
1,563
Eneo la upanuzi lililopandwa miti 2012/2013 – 2015/2016
1,157
Jumla la eneo lilipandwa miti
2,720
Eneo la upanuzi ambao halijapandwa miti(makadirio)
471
Jumla kuu
3,191
Eneo la msitu wa asili ni hekta 1,572 na eneo hili limejumuisha maeneo yenye vyanzo vya maji.

Kwa ajili ya usimamizi shamba limegawanywa katika sehemu sita zinazojulikana kama Safu. Shamba hili linaongozwa na Meneja wa shamba ambaye anawajibika kwa Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misistu Tanzania (TFS).Meneja wa Shamba ana meneja msaidizi. Safu husimamiwa na wakuu wa safu.Hawa pamoja na wakuu wa vitengo mbalimbali kama vile Uvunaji na leseni, Miundombinu, Ulinzi wa msitu na Nyuki,Uhasibu na Ugavi huwajibika kwa meneja wa Shamba.

Shamba lina watumishi wa kudumu 34 wa kada mbalimbali na watumishi wa mkataba 9, Maafisa misitu (4), Wasaidizi Misitu wa Stashahada na Astashahada (7), Wasaidizi Misitu (20), Mhasibu (1), Katibu Muhtasi (1) na Tabibu (1).Aidha kutokana na ufinyu wa watumishi tuna watumishi wanaofanya kazi kwa mkataba wa mwaka mmoja mmoja ambao ni madereva (2), Walinzi (6), Fundi bomba (1).

Shamba lina mpango wa Usimamizi (Management Plan) wa kipindi cha miaka mitano.Mpango huo wa usimamizi ndio mwongozo wa kuendesha Shamba na kuandaa mipango kazi na bajeti za kila mwaka (Annual Plan of Operations). Mpango wa usimamizi wa sasa ulianza 2012/2013 hadi 2017/2018.
Mpango huu unahusisha kazi zifuatazo
  • ·       Kazi za shambani (Ukuzaji wa miche ya miti katika bustani iliyopo Kawetire na Mbeya Peak) kuandaa mashamba kwa ajili ya upandaji miti katika maeneo yaliyovunwa na katika maeneo ya upanuzi (Extension area), Upandaji miti,usafi wa mashamba (sanitary slashing), kupogoa matawi, doria kwa ajili ya ulinzi wa msitu,ujenzi na ukarabati wa barabara za msituni na uvunaji miti.
  • Kazi za utawala na mafunzo (Mikutano, Mafunzo ya muda mfupi, safari za kikazi, likizo za watumishi, ujenzi na ukarabati wa majengo na nyumba za kuishi watumishi, uendeshaji wa magari,manunuzi mbalimbali na kazi za utawala kwa ujumla)
Katika mwaka wa fedha 2012/2013 Jumla ya hekta 275 zilipandwa kwenye maeneo ya upanuzi na hekta 95 kwenye maeneo yaliyovunwa miti.Hii inafanya jumla ya eneo lililopandwa kwa mwaka huo kuwa hekta 370.

Katika mwaka wa fedha 2013/2014 Jumla ya hekta 165 zilipandwa katika maeneo ya upanuzi katika Safu ya Lwanjiro na Ipinda na hekta 129 zilipandwa katika maeneo yaliyovunwa katika safu za Kawetire na Ipinda.

Kwa kipindi cha miaka mitatu ya fedha tumekuwa tukivuka lengo la upandaji kwani katika mwaka wa fedha 2012/2013 upandaji ulikuwa 149%. Kwa mwaka wa fedha 2013/2014 upandaji ulikuwa 156.5% na 2014/2015 upandaji ulikuwa 112% haya ni mafanikio makubwa kwa shamba na Wakala kwa ujumla.

Changamoto iliyopo ni kuhakikisha kwamba nguvu na gharama kubwa iliyotumika kwa ajili ya upandaji miti haipotei.Tumeweka mikakati ya kuhakikisha miti inatunzwa kwa uangalizi wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha tunafanya usimamizi wa karibu ili kuilinda miti.

Shamba la miti kawetire tumekuwa tukikusanya maduhuri ya serikali yanayotokana na uuzaji wa miti ambapo   mwenendo wa ukusanyaji  maduhuri ni kama ifuatavyo. 
FY
Volume
TOTAL
2012/13
        6,867
       344,968,053
2013/14
      17,636
       823,327,314
2014/15
      17,737
       882,335,080
2015/16
      12,168
       498,150,755
TOTAL
      54,408
   2,548,781,202

Katika shamba la miti Kawetire tumeanzisha mradi wa ufugaji nyuki na hadi sasa tuna mizinga ipatayo 100 kati ya hiyo mizinga  yenye nyuki kwa sasa ni 31.
   
Katika taarifa za miaka iliyopita moja kati ya changamoto ambazo zimekuwa zikionekana kwenye taarifa hizo ni uchakavu wa nyumba za watumishi, na baadhi ya nyumba hizo zilijengwa mwaka 1937, kimsingi nyumba ni chakavu na nyingi zinahitaji kubomolewa kwani hazifai tena kufanyiwa ukarabati.Kwa nyumba ambazo zina unafuu wa kufanyia ukarabati, tumefanikiwa kufanya ukarabati mkubwa na mdogo pamoja na ujenzi wa vyoo. Ukarabati huu unaendelea kufanyika kadri bajeti inavyoruhusu. Hii ni katika kuhakikisha kwamba watumishi wanaishi katika mazingira ya kuridhisha na masafi.

Pamoja na shughuli za upandaji miti na shughuli mbalimbali shamba linawezesha na kutoa huduma mbalimbali kwa jamii inayozunguka shamba na taifa kwa ujumla.Uwezeshaji na huduma hizi ni kama ifuatavyo;

Shamba linaajiri vibarua wa kutwa zaidi ya 600 kwa mwaka kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za shamba, vibarua wengi huajiriwa wakati wa upandaji miti, kutengeneza barabara za moto na ulinzi wa misitu; wengi wa vibarua ni wenyeji wa mbeya kutoka vijiji vinavyozunguka shamba.

Wafanyakazi wa shamba na wanavijiji hugawiwa maeneo ya kulima katika maeneo yaliyovunwa miti. Wastani wa watu 300 hufaidika na huduma hiyo ambayo utaratibu huu hutoa mchango kwenye usalama wa chakula (food security) na kuongezea wananchi mapato.

Wananchi waishio jirani na shamba huruhusiwa kuokota kuni kavu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Wananchi wanaruhusiwa pia kutafuta mboga katika maneo ya msitu.

Shamba la Miti Kawetire linatoa mchango katika huduma za afya na maendeleo ya wananchi kwa ujumla. Kuna zahanati moja ambayo hutoa huduma ya matibabu kwa wanavijiji na watumishi wa shamba. Zahanati hii imekuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha huduma za afya za watumishi na wanavijiji wa jirani zinaimarika kwa kutoa elimu juu ya lishe bora na elimu ya kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi (VVU).

Shamba pia linachangia katika sekta ya ujenzi kutokana  na mauzo ya miti ambayo inachanwa mbao zinazotumika kwenye ujenzi.

Katika kuunga mkono agizo la Mh. Raisi wa Jamhuri ya Mungao wa Tanzania kwamba lazima kila mtoto akalie dawati Shamba la Miti Kawetire limeanza kutengeneza madawati 264 ambayo yatagawanywa katika Shule mbalimbali za Wilaya ya Mbeya.

Changamoto mbalimbali zinazolikabili shamba ambazo ni pamoja na:-
Kusitishwa kwa upandaji wa eneo la upanuzi safu ya Karuwe
Eneo hili lilikuwa ndani hifadhi yam situ wa safu ya mlima mbeya lenye ukubwa wa hekta 1280. Eneo hili likuwa  linavamiwa na wananchi mara kwa mara  na kufanywa eneo la malisho, kilimo na uwindaji hivyo kupelekea matumizi ya moto wakati wakiendesha shughuli zao na kusababisha mioto ya mara kwa mara na hivyo kuharibu uoto uliokuwepo.

Kutokana na sababu hiyo eneo hilo lilihamishwa kutoka kwenye usimamizi wa Kanda na kuhamishiwa kwa Shamba la Miti Kawetire kwa ajili ya kupanda miti ili kurudishia uoto uliokuwepo, hii ilikuwa ni pamoja na kupanda miti ya kibiashara na kuhakikisha kwamba Sheria ya mazingira inafuatwa kwa kuacha vyanzo vya maji umbali wa mita 60 au zaidi.

Upandaji huu ulizingatia kwamba, maeneo yaliyo mbali na vyanzo vya maji yapandwe miti ya kibiashara na yale yaliyo karibu na vyanzo vya maji yapandwe miti rafiki ifaayo maeneo hayo ikiwamo na utunzaji vyanzo hivyo.

Upandaji ulianza Januari 2016 na baada ya kupanda hekta 295 kati ya 478 zilizotakiwa kupandwa 2015/2016, tulipata zuio kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwamba tusiendelea kupanda wala kuhudumia miti iliyokwishapandwa kwani kulikuwa na malalamiko kutoka Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira ya jiji la Mbeya kwamba tunaharibu vyanzo vya maji.

Shamba la miti kawetire hupata matukio ya moto ambao kwa kiasi kikubwa husababishwa na shughuli zinazofanywa na wananchi wanaozunguka msitu kama vile uwindaji, uandaaji wa mashamba na kurina asali. Matukio haya hupunguza jitihada za usimamizi endelevu wa shamba.

Katika kukabiliana na changamoto hii uongozi wa shamba la miti kawetire umekuwa ukifanya yafuatayo;
Kuelimisha jamii 
  • Vijiji kumi na sita vinavyozunguka Shamba hupewa elimu ya kuzuia na kupambana na moto kwa njia ya mikutano ya kampeni ya kudhibiti moto
  • Kikosi maalumu cha kupambana na moto  kinachofanya kazi saa 24 kwa siku kwa kipindi chote cha kiangazi
  • Kutengeneza barabara za kinga dhidi ya moto kuzunguka shamba lote kila mwaka
  • Kuchoma barabara za moto wakati ambapo nyasi hazijakauka sana ili kupunguza kasi ya moto pale unapotokea.
  • Kuweka ratiba kwa watumishi wote wa shamba kuwa tayari kupambana na moto pale unapotokea.
Shamba halina lori wala “tractor” kwa ajili ya kusaidia shughuli za bustani na upandaji jambo ambalo linafanya usafirishaji wa miche kwenda maeneo ya upandaji kuwa mgumu na kuchukua muda mrefu kwani wakati mwingine tunalazimika kutumia “L/c hardtop”
Ili kukabiliana na changamoto hii, katika mwaka wa fedha 2015/2016 shamba lilitenga bajeti kwa ajili ya kununua grader na tractor na mchakato wa manunuzi unaendelea na unafanyika na TFS HQ

Shamba lina upungufu wa watumishi wa kada mbalimbali hasa madereva na walinzi.
Ili kukabiliana na changamoto hii shamba huajiri vibarua kwa mkataba wakati tukisubiri ajira za kudumu kutoka Serikalini.

Majengo na nyumba za watumishi zimechakaa kwani nyingi zimejengwa mwaka 1937.Nyumba nyingine hazifai hata kufanyiwa ukarabati kwani zimeanza kubomoka na kuta kuanza kudondoka.

Katika kukabiliana na changamoto hii pamoja na ufinyu wa bajeti Shamba limeweza kufanya ukarabati mkubwa wa majengo mawili ,nyumba ishirini na mbili za watumishi, ujenzi wa vyoo, majiko na ujenzi wa nyumba mbili za watumishi hii imepelekea kubadilisha muonekano wa mandhari ya nyumba na ofisi.
Eneo la msitu wa nishati wa mbeya (Mbeya fuel wood) lililokuwa na zaidi ya hekta 300 limekuwa likivamiwa na kupimwa viwanja na mpaka sasa eneo lililobaki ni kama hekta 67 tu.

Katika kukabiliana na changamoto hii na kulinusuru eneo lilobaki uongozi wa Shamba umelipima eneo kwa kushirikiana na Ofisi ya Kanda ya Nyanda za juu Kusini na Halmashauri ya jiji la Mbeya katika kuandaa mpango kabambe ili kuinua utalii wa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini. Kazi hii inaendelea na ipo katika hatua ya upimaji na upangaji wa viwanja kwa ajili ya makazi, mahoteli, nyumba za ibada, viwanja vya michezo na maeneo yatakayo hifadhiwa.
Share:

Sunday, February 5, 2017

TFS YATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU KUWEKA BEACONS KWENYE HIFADHI

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo akishiriki zoezi linaloendelea nchi nzima la kuweka mawe ya alama (beacons) kwenye mipaka ya Shamba la Miti la Mtibwa mwishoni mwa wiki alipopita ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliyetoa miezi miwili na siku tisa kwa Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Misitu kuhakikisha wanaweka becons kwenye mipaka yao ili kuepusha migogoro na wanavijiji wanaowazunguka. Wanaomtazama ni baaadhi ya watendaji wa Shamba la Miti la Mtibwa waliokuwa wakitekeleza agizo hilo kabla ya mtendaji huyo kuungana nao.


Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetekeleza azigo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka wakuu wa mapori ya hifadhi za misitu kuhakikisha wanaweka mawe ya alama kwenye mipaka yao kuepusha migogoro na wanavijiji wanaowazunguka.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo mwishoni mwaka jana alipokuwa akizungumza na watendaji wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na wakuu wa mapori ya hifadhi za misitu nchini katika kikao alichokiitisha kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, mjini Dodoma.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo akizungumza na watendaji wa Shamba la Miti la Mtibwa mwisahoni mwa wiki alisema miongoni mwa maagizo Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizindua Bunge tarehe 20 Novemba, 2015 ni kuanisha mipaka, kupambana na ujangili na kukusanya mapato na Mwaka jana Mheshimiwa Waziri Mkuu ameagizo kuweka beacons kwenye hifadhi zote za misitu.

“Nataka kuwahakikishia mpaka sasa tunapozungumza tumeshatekeleza agizo la Mhe. Waziri Mkuu kuweka beacons kwenye hifadhi zote za misitu si katika Shamba la Miti la Mtibwa pekee,” alisema.

Katika ziara hiyo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo alishiriki zoezi la kuweka mawe ya alama (beacons) kwenye mipaka ya Shamba la Miti la Mtibwa kuonyesha nia ya dhati ya Wakala kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliyetoa miezi miwili na siku tisa kwa Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Misitu kuhakikisha wanaweka becons kwenye mipaka yao ili kuepusha migogoro na wanavijiji wanaowazunguka.
Aidha, mtendaji huyo aliwataka watendaji wake kuhakikisha wanakamilisha zoezi hilo mapema iwezekanavyo na kurudi kuwambia wananchi mipaka yao iko wapi.

“Zoezi hili lisisishie kuweka alama hizi tu, waonyesheniwananchi ukomo ni wapi. ninyi mnatambua mipaka yenu iko wapi kwa hiyo waelewesheni wananchi kwa kuwaonyesha alama hizi tulizoziweka nchi nzima.” Alisema.

Aidha, Pro. Silayo aliwataka watendaji hao mara baada ya kuweka alama za mipaka wawaeleze wananchi ni umbali gani wanapaswa waache kutoka kwenye hizo alama na kuwaelimishe kwamba hiyo ndiyo buffer zone.

“Kila mmoja anayo fursa ya kuitisha mkutano na wananchi na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kuwa na mapori ya akiba. Pandeni kwenye majukwaa, muelezee mipaka hiyo mipya na wananchi watawaelewa kwa sababu mwenye dhamana ya kwanza katika kutoa elimu hii ni sisi wakala,” alisistiza.
Share:

Friday, February 3, 2017

International Day of Forests 2017

Search This Blog

Powered by Blogger.