• This is default featured slide 1 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 2 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 3 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 4 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

  • This is default featured slide 5 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday, March 9, 2017

UUZAJI WA MITI YA MISAJI KWA NJIA YA MAKUBALIANO BINAFSI (PRIVATE AGREEMENT) KATIKA SHAMBA LA MITI MTIBWA, MOROGORO NA LONGUZA, MUHEZA TANGA


1.    Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unatarajia kuuza miti aina ya Misaji yenye jumla ya meta za ujazo 10,800.420 iliyopo mashamba ya miti ya Mtibwa na Longuza yaliyopo mikoa ya Morogoro na Tanga mtawalia. Mauzo haya yatafanyika Machi 21, 2017 katika chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya BUSTANI kilichopo katika makutano ya Mtaa wa Shaaban Robert/Samora Avenue mjini Dar es Salaam saa nne na nusu (4:30) asubuhi. Uuzaji huu utafanyika kwa njia ya makubaliano binafsi (private agreement) kwa kuzingatia kanuni 31 (iii) ya kanuni za sheria ya misitu za mwaka 2004. Miti hii ya misaji itauzwa mahali ilipo na jinsi ilivyo na mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.

2.    Kampuni au mtu binafsi anayetaka kushiriki mauzo kwa njia ya makubaliano binafsi anatakiwa kuwasilisha maombi kwenye bahasha iliyofungwa kuonesha nia ya kushiriki mauzo kwa njia ya makubaliano binafsi akiambatisha leseni ya biashara, Usajili wa kiwanda cha kuchakata magogo (2016/17), usajili wa biashara ya mazao ya Misitu (2016/2017) na cheti cha utambulisho wa mlipa kodi (TIN). Aidha, anatakiwa aoneshe jina la shamba, jina la kiunga, namba ya kitalu/vitalu na ujazo anaotarajia kununua kama ilivyo kwenye jedwali namba 1 na 2 hapo chini,

3.    Baada ya kuwasilisha maombi hayo mnunuzi ataitwa kwenye majadiliano (negotiation) na Wakala wa Huduma za misitu Tanzania. Maafikiano yakifikiwa, mnunuzi ataelekezwa kufanya malipo kama inavyooneshwa katika kipengele Na. 9. Baada ya malipo hayo mnunuzi ataingia mkataba wa kisheria wa manunuzi ya miti ya misaji kati yake na TFS.

4.    Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unawaalika wanunuzi kutuma maombi yao kwa ajili ya kufanya majadiliano ya kununua miti ya misaji kwa njia ya makubaliano binafsi ambapo mnunuzi anaweza kuchagua viunga vifuatavyo;

JEDWALI Na. 1: KIUNGA NAMBA KH2B NA KH2C SHAMBA LA MITI LONGUZA
Na.
Jina la Kitalu
Ujazo kwa kitalu (m3)
Bei ya awali/kitalu/m3
1
KH 2B-PA04
403.620
750,000
2
KH 2B-PA06
401.404
750,000
3
KH 2B-PA08
452.352
750,000
4
KH 2B-KW 1
741.714
750,000
5
KH 2B-KW 2
243.000
750,000
6
KH 2B-KW 3
303.593
900,000
7
KH 2B-KW 4
307.872
900,000
8
KH 2C-01
549.727
900,000
9
KH 2C-02
663.417
900,000
10
KH 2C-03
597.021
900,000
11
KH 2C-04
641.215
900,000
12
KH 2C-05
201.759
900,000
Jumla ya ujazo
5,506.690




JEDWALI Na. 2: KIUNGA NAMBA MT 11 SHAMBA LA MITI MTIBWA
Na.
Jina la kitalu
Ujazo wa kitalu (m3)
Bei ya awali/kitalu/m3
1
MT 11- C8
400.05

2
MT 11-D1
344.366
700,000
3
MT 11- D2
415.078
700,000
4
MT 11- D3
397.646
700,000
5
MT 11- D4
300.512
700,000
6
MT 11- D5
203.485
700,000
7
MT 11- D6
203.876
700,000
8
MT 11- D7
301.206
700,000
9
MT 11- D8
200.162
700,000
10
MT 11- D9
203.434
700,000
11
MT11-T1
201.434
700,000
12
MT11-T2
200.000
700,000
13
MT11-T3
301.064
700,000
14
MT11-T4
200.052
700,000
15
MT11-T5
201.271
700,000
16
MT11-T6
214.993
700,000
17
MT11-T7
218.993
700,000
18
MT11-T8
159.277
700,000
19
MT11-J1
300.201
700,000
20
MT11-J2
326.625
700,000
Jumla ya Ujazo
5,293.725




5.    Mnunuzi atakayefanikiwa kununua miti ya misaji hataruhusiwa kusafiirisha magogo nje ya nchi kwa mujibu wa kanuni ya 50(1) ya mwaka 2004. Kusafirisha Mazao ya Misitu nje ya nchi ni baada ya kuyachakata kwa Mujibu wa Tangazo la Serikali Na 69 la mwaka 2006.

6.     Makampuni na watu binafsi wanakaribishwa kutembelea viunga shambani wakati wa saa za kazi kuanzia saa tatu (3:00) asubuhi hadi saa tisa (9:00) alasiri isipokuwa siku za sikukuu. Meneja wa shamba au msaidizi wake atakuwepo kwa ajili ya maelekezo zaidi.

7.    Wanunuzi wanapaswa kuchukua na kusoma masharti ya uvunaji kwa kila shamba. Masharti hayo yanapatikana ofisi za shamba husika.

8.     Bei ya kianzio kwa mita moja ya ujazo imeoneshwa katika Jedwali namba 1 na 2 hapo juu ikijumuisha ‘VAT’, ‘CESS’ na ‘LMDA’.
9.    Mnunuzi atakayeshinda atatakiwa kulipa asilimia ishirini na tano (25%) ya thamani yote ya mazao ya misitu aliyonunua siku tatu (3) baada ya makubaliano kufanyika. Fedha hizo hazitarudishwa iwapo mnunuzi ataghairi. Asilimia sabini na tano (75%) iliyobaki italipwa ndani ya miezi miwili baada ya kusaini mkataba wa mauziano na Wakala. Malipo yatafanyika katika Akaunti ya shamba la Miti husika kama inavoonekana hapa chini;

  1. SHAMBA LA MITI MTIBWA,                                ii. SHAMBA LA MITI LONGUZA,
AKAUNTI NA. 22010000567                                    AKAUNTI NA. 41901000015
NMB – TURIANI                                                          NMB – MUHEZA
10. Mnunuzi atapaswa kuwasilisha hati ya malipo (pay – in – slip) ya benki kwa meneja wa shamba kama uthibitisho wa malipo si zaidi ya siku tatu (3) baada ya malipo kufanyika.

11. Mteja atatakiwa kuondoa mazao ya misitu aliyonunua ndani ya miezi miwili baada ya kumaliza kulipa malipo yote kwa asilimia 100.
12. Tangazo hili pia linapatikana katika tovoti zifuatazo za Wakala na Wizara: www.tfs.go.tz, na www.mnrt.go.tz

13. Maombi yote yawasilishwe siku ya mauzo kabla ya saa 4:00 asubuhi. wanunuzi watakaochelewa kuwasilisha maombi yao kwa siku na muda uliopangwa hawataruhusiwa kushiriki katika majadiliano ya mauzo.


limetolewa na
MTENDAJI MKUU
S.L.B 40832,

DAR ES SALAAM.
Share:

International Day of Forests 2017

Search This Blog

Powered by Blogger.