Wednesday, March 1, 2017

SERIKALI YAZUIA USAFIRISHAJI WA MKAA NJE YA WILAYA

Mkaa ukiwa unasafirishwa toka eneo moja kwenda jingine

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amepiga marufuku usafirishaji wa mkaa nje ya wilaya iliyouzalisha.

Ametoa tamko hilo alipokuwa akifungua mkutano wa tano wa Baraza la Wafanyakazi la wakala wa Huduma za Misitu(TFS) mjini Dodoma.

“Kuanzia sasa kibali cha kukata miti kwa ajili ya mkaaa kitolewe na kusimamia kuwa mkaa unaokatwa na kuchomwa ndani ya wilaya utumike ndani ya wilaya hiyo tu! Hakuna kusafirisha nje ya wilaya, agizo hili lianze kutekekelezwa kuanzia Leo tarehe 28/02/2017," amesema Mhe. Magembe.

Katika harakati za kupamabana na biashara ya usafirishaji mkaa, Mhe. Maghembe ameagiza Wakuu wa Wilaya kurudishwa katika Kamati za Uvunaji za Wilaya zenye jukumu la kugawa mazao ya misitu kwa kuzingatia Mpango wa Uvunaji ulioandaliwa na Afisa Misitu na Meneja wa Misitu wa wilaya husika.
Share:

0 comments:

Post a Comment

International Day of Forests 2017

Search This Blog

Powered by Blogger.