1. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unatarajia kuuza miti
aina ya Misaji yenye jumla ya meta za ujazo 10,800.420 iliyopo mashamba ya miti ya Mtibwa na Longuza yaliyopo
mikoa ya Morogoro na Tanga mtawalia. Mauzo haya yatafanyika Machi 21, 2017 katika
chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya BUSTANI kilichopo katika makutano ya Mtaa
wa Shaaban Robert/Samora Avenue mjini Dar es Salaam saa nne na nusu (4:30)
asubuhi. Uuzaji huu utafanyika kwa njia ya makubaliano binafsi (private
agreement) kwa kuzingatia kanuni 31 (iii) ya kanuni za sheria ya misitu za
mwaka 2004. Miti hii ya misaji itauzwa mahali ilipo na jinsi ilivyo na
mnunuzi hatakuwa na haki ya kudai fidia baada ya mauzo.
2. Kampuni au mtu binafsi anayetaka kushiriki mauzo kwa njia ya
makubaliano binafsi anatakiwa kuwasilisha maombi kwenye bahasha iliyofungwa
kuonesha nia ya kushiriki mauzo kwa njia ya makubaliano binafsi akiambatisha
leseni ya biashara, Usajili wa kiwanda cha kuchakata magogo (2016/17), usajili
wa biashara ya mazao ya Misitu (2016/2017) na cheti cha utambulisho wa mlipa
kodi (TIN). Aidha, anatakiwa aoneshe jina la shamba, jina la kiunga, namba ya
kitalu/vitalu na ujazo anaotarajia kununua kama ilivyo kwenye jedwali namba 1
na 2 hapo chini,
3. Baada ya kuwasilisha maombi hayo mnunuzi ataitwa kwenye
majadiliano (negotiation) na Wakala wa Huduma za misitu Tanzania. Maafikiano yakifikiwa,
mnunuzi ataelekezwa kufanya malipo kama inavyooneshwa katika kipengele Na. 9. Baada ya malipo hayo mnunuzi
ataingia mkataba wa kisheria wa manunuzi ya miti ya misaji kati yake na TFS.
4. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania unawaalika wanunuzi kutuma
maombi yao kwa ajili ya kufanya majadiliano ya kununua miti ya misaji kwa njia
ya makubaliano binafsi ambapo mnunuzi anaweza kuchagua viunga vifuatavyo;
JEDWALI
Na. 1: KIUNGA NAMBA KH2B NA KH2C SHAMBA LA MITI LONGUZA
Na.
|
Jina la Kitalu
|
Ujazo kwa kitalu (m3)
|
Bei ya awali/kitalu/m3
|
1
|
KH 2B-PA04
|
403.620
|
750,000
|
2
|
KH 2B-PA06
|
401.404
|
750,000
|
3
|
KH 2B-PA08
|
452.352
|
750,000
|
4
|
KH 2B-KW 1
|
741.714
|
750,000
|
5
|
KH 2B-KW 2
|
243.000
|
750,000
|
6
|
KH 2B-KW 3
|
303.593
|
900,000
|
7
|
KH 2B-KW 4
|
307.872
|
900,000
|
8
|
KH 2C-01
|
549.727
|
900,000
|
9
|
KH 2C-02
|
663.417
|
900,000
|
10
|
KH 2C-03
|
597.021
|
900,000
|
11
|
KH 2C-04
|
641.215
|
900,000
|
12
|
KH 2C-05
|
201.759
|
900,000
|
Jumla ya
ujazo
|
5,506.690
|
|
|
|
|
|
JEDWALI
Na. 2: KIUNGA NAMBA MT 11 SHAMBA LA MITI MTIBWA
Na.
|
Jina la kitalu
|
Ujazo wa kitalu (m3)
|
Bei ya awali/kitalu/m3
|
1
|
MT 11- C8
|
400.05
|
|
2
|
MT 11-D1
|
344.366
|
700,000
|
3
|
MT 11- D2
|
415.078
|
700,000
|
4
|
MT 11- D3
|
397.646
|
700,000
|
5
|
MT 11- D4
|
300.512
|
700,000
|
6
|
MT 11- D5
|
203.485
|
700,000
|
7
|
MT 11- D6
|
203.876
|
700,000
|
8
|
MT 11- D7
|
301.206
|
700,000
|
9
|
MT 11- D8
|
200.162
|
700,000
|
10
|
MT 11- D9
|
203.434
|
700,000
|
11
|
MT11-T1
|
201.434
|
700,000
|
12
|
MT11-T2
|
200.000
|
700,000
|
13
|
MT11-T3
|
301.064
|
700,000
|
14
|
MT11-T4
|
200.052
|
700,000
|
15
|
MT11-T5
|
201.271
|
700,000
|
16
|
MT11-T6
|
214.993
|
700,000
|
17
|
MT11-T7
|
218.993
|
700,000
|
18
|
MT11-T8
|
159.277
|
700,000
|
19
|
MT11-J1
|
300.201
|
700,000
|
20
|
MT11-J2
|
326.625
|
700,000
|
Jumla ya
Ujazo
|
5,293.725
|
|
5.
Mnunuzi atakayefanikiwa kununua miti ya misaji hataruhusiwa
kusafiirisha magogo nje ya nchi kwa mujibu wa kanuni ya 50(1) ya mwaka 2004.
Kusafirisha Mazao ya Misitu nje ya nchi ni baada ya kuyachakata kwa Mujibu wa
Tangazo la Serikali Na 69 la mwaka 2006.
6.
Makampuni na watu binafsi wanakaribishwa
kutembelea viunga shambani wakati wa saa za kazi kuanzia saa tatu (3:00)
asubuhi hadi saa tisa (9:00) alasiri isipokuwa siku za sikukuu. Meneja wa
shamba au msaidizi wake atakuwepo kwa ajili ya maelekezo zaidi.
7.
Wanunuzi
wanapaswa kuchukua na kusoma masharti ya uvunaji kwa kila shamba. Masharti hayo
yanapatikana ofisi za shamba husika.
8. Bei ya kianzio kwa mita moja ya ujazo
imeoneshwa katika Jedwali namba 1 na 2 hapo juu ikijumuisha ‘VAT’, ‘CESS’ na
‘LMDA’.
9.
Mnunuzi
atakayeshinda atatakiwa kulipa asilimia ishirini na tano (25%) ya thamani yote
ya mazao ya misitu aliyonunua siku tatu (3) baada ya makubaliano kufanyika.
Fedha hizo hazitarudishwa iwapo mnunuzi ataghairi. Asilimia sabini na tano
(75%) iliyobaki italipwa ndani ya miezi miwili baada ya kusaini mkataba wa
mauziano na Wakala. Malipo yatafanyika katika Akaunti ya shamba la Miti husika
kama inavoonekana hapa chini;
- SHAMBA LA MITI MTIBWA, ii. SHAMBA
LA MITI LONGUZA,
AKAUNTI NA. 22010000567 AKAUNTI NA. 41901000015
NMB – TURIANI NMB – MUHEZA
10.
Mnunuzi
atapaswa kuwasilisha hati ya malipo (pay – in – slip) ya benki kwa meneja wa
shamba kama uthibitisho wa malipo si zaidi ya siku tatu (3) baada ya malipo
kufanyika.
11. Mteja
atatakiwa kuondoa mazao ya misitu aliyonunua ndani ya miezi miwili baada ya
kumaliza kulipa malipo yote kwa asilimia 100.
12.
Tangazo
hili pia linapatikana katika tovoti zifuatazo za Wakala na Wizara: www.tfs.go.tz,
na www.mnrt.go.tz
13.
Maombi
yote yawasilishwe siku ya mauzo kabla ya saa 4:00 asubuhi. wanunuzi
watakaochelewa kuwasilisha maombi yao kwa siku na muda uliopangwa
hawataruhusiwa kushiriki katika majadiliano ya mauzo.
limetolewa
na
MTENDAJI MKUU
S.L.B 40832,
DAR ES SALAAM.
0 comments:
Post a Comment