Thursday, March 2, 2017

Menejimenti ya Wakala wa Humuma za Misitu yakutana Jijini Dodoma kujadili namna ya kuanzisha kikosi cha intelijensia

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kazi cha Menejimenti ya TFS Makao Makuu, Meneja wa Kanda, Mashamba ya Miti na Wakuu wa FSU katika Ukumbi wa Hazina Dodoma.

Lengo kuu la mkutano huo ni kuanzisha kikosi cha intelijensia ili kupunguza matumizi katika doria na kupata taaarifa za kimkakati zitakazopunguza uvamizi katika misitu.

“Tuanzishe Kikosi cha Intelegensia kitakachohakikisha kinaboresha ukuaji wa sekta ya misitu nchini,” alisema Prof. Silayo
 

Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali Misitu wa TFS, Mohammed Kilongo, akizungumza katika Mkutano huo ambapo alieleza umuhimu wa kuanzishwa Kikosi cha Intelegensia katika kuendeleza Misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimfuatilia kwa umakini Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo alipokuwa akihutubia kwenye mkutano huo.

Share:

0 comments:

Post a Comment

International Day of Forests 2017

Search This Blog

Powered by Blogger.