Sunday, February 5, 2017

TFS YATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU KUWEKA BEACONS KWENYE HIFADHI

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo akishiriki zoezi linaloendelea nchi nzima la kuweka mawe ya alama (beacons) kwenye mipaka ya Shamba la Miti la Mtibwa mwishoni mwa wiki alipopita ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliyetoa miezi miwili na siku tisa kwa Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Misitu kuhakikisha wanaweka becons kwenye mipaka yao ili kuepusha migogoro na wanavijiji wanaowazunguka. Wanaomtazama ni baaadhi ya watendaji wa Shamba la Miti la Mtibwa waliokuwa wakitekeleza agizo hilo kabla ya mtendaji huyo kuungana nao.


Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetekeleza azigo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka wakuu wa mapori ya hifadhi za misitu kuhakikisha wanaweka mawe ya alama kwenye mipaka yao kuepusha migogoro na wanavijiji wanaowazunguka.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo mwishoni mwaka jana alipokuwa akizungumza na watendaji wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na wakuu wa mapori ya hifadhi za misitu nchini katika kikao alichokiitisha kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, mjini Dodoma.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo akizungumza na watendaji wa Shamba la Miti la Mtibwa mwisahoni mwa wiki alisema miongoni mwa maagizo Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizindua Bunge tarehe 20 Novemba, 2015 ni kuanisha mipaka, kupambana na ujangili na kukusanya mapato na Mwaka jana Mheshimiwa Waziri Mkuu ameagizo kuweka beacons kwenye hifadhi zote za misitu.

“Nataka kuwahakikishia mpaka sasa tunapozungumza tumeshatekeleza agizo la Mhe. Waziri Mkuu kuweka beacons kwenye hifadhi zote za misitu si katika Shamba la Miti la Mtibwa pekee,” alisema.

Katika ziara hiyo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo alishiriki zoezi la kuweka mawe ya alama (beacons) kwenye mipaka ya Shamba la Miti la Mtibwa kuonyesha nia ya dhati ya Wakala kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliyetoa miezi miwili na siku tisa kwa Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Misitu kuhakikisha wanaweka becons kwenye mipaka yao ili kuepusha migogoro na wanavijiji wanaowazunguka.
Aidha, mtendaji huyo aliwataka watendaji wake kuhakikisha wanakamilisha zoezi hilo mapema iwezekanavyo na kurudi kuwambia wananchi mipaka yao iko wapi.

“Zoezi hili lisisishie kuweka alama hizi tu, waonyesheniwananchi ukomo ni wapi. ninyi mnatambua mipaka yenu iko wapi kwa hiyo waelewesheni wananchi kwa kuwaonyesha alama hizi tulizoziweka nchi nzima.” Alisema.

Aidha, Pro. Silayo aliwataka watendaji hao mara baada ya kuweka alama za mipaka wawaeleze wananchi ni umbali gani wanapaswa waache kutoka kwenye hizo alama na kuwaelimishe kwamba hiyo ndiyo buffer zone.

“Kila mmoja anayo fursa ya kuitisha mkutano na wananchi na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kuwa na mapori ya akiba. Pandeni kwenye majukwaa, muelezee mipaka hiyo mipya na wananchi watawaelewa kwa sababu mwenye dhamana ya kwanza katika kutoa elimu hii ni sisi wakala,” alisistiza.
Share:

0 comments:

Post a Comment

International Day of Forests 2017

Search This Blog

Powered by Blogger.